Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Liberatus Sabas ameongoza operesheni katika Wilaya ya Kibiti, Kijiji cha Rungungu eneo ambalo mauaji yalilindima na kutikisa Mkoa wa Kipolisi Rufiji katika Wilaya ya Ikwiriri,Mkuranga na Kibiti eneo ambalo lilikabiliwa na mauaji ya Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kisiasa, Askari Polisi pamoja na watumishi wengine wa Serikali.

Mauaji hayo yaliendeshwa na kikundi cha kiarifu ambacho kiliamua kujichukulia eneo katika kijiji cha Rungungu walilotumia kama eneo la makazi na mazoezi kabla hawajaenda kutimiza azima yao ya uharifu.Katika hatua hiyo Kamishna CP Sabas amesema Jeshi la Polisi kwa
kushirikiana na Vyombo vingine ya Ulinzi na Usalama na kuweza kufanikiwa kulitokomeza kundi hilo la kihalifu ambalo lilikuwa limeweka himaya katika mapori hayo, ameongezea kwa kusema katika Operesheni iliyofanywa katika eneo hilo wamehakikisha pori hilo liko salama na hakuna kitu chochote walichoweza kukipata porini humo.

Latest News

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:24 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:23 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Chanjo ya Surua Rubella yatolewa Singida.
18 Jun 2019 08:52 - Kisali Shombe

Zaidi ya asilimia 80 ya  watoto  wenye umri wa chini ya miaka mitano, wamepatiwa chanjo ya  Surua Rubella  katika ha [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.