Star Tv

Watawala wa kijeshi wa Sudan na viongozi wa vuguvugu la maandamano wamekubaliana juu ya kuundwa kwa utawala wa mpito wa miaka mitatu, ambao utakabidhi madaraka kamili kwa raia.

Mjumbe wa baraza la kijeshi linaloongoza nchi hiyo, Luteni Jenerali Yasser al-Atta ametangaza muafaka huo muda mfupi uliopita mbele ya waandishi wa habari. Al-Atta amesema makubaliano ya mwisho ya kugawana madaraka, na kuundwa kwa taasisi za uongozi wa mpito yatatiwa saini baina ya wanajeshi na waandamanaji katika muda usiozidi saa 24, chini ya masharti yanayokidhi matakwa ya umma wa Sudan. Afisa huyo amesema miezi sita ya kwanza itatengwa maalum kufikia makubaliano ya amani na makundi ya waasi ndani ya nchi hiyo. Amesema pia kuwa bunge la mpito litakuwa na viti 300, asilimia 67 ya viti hivyo ikikaliwa na wanachama wa vuguvugu la waandamanaji lijulikanalo kama ''Muungano kwa ajili ya Uhuru na Mabadiliko''.

 

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.