Star Tv

Apple imekuwa ni kampuni ya umma ya kwanza duniani kuwa na thamani ya dola trilioni moja($1 trillion), (£767bn).Thamani ya soko la wathengezaji wa iPhone imefikia kiwango hicho mjini in New York Alhamisi na hisa zake zilifikia rekodi mpya ya $207.39.

Hisa zake zimekuwa zikipanda tangu Jumanne wakati kampuni hiyo iliporipoti kupata matokeo mazuri kuliko ilivyotarajiwa katika kipindi cha miezi mitatu kuelekea mwezi Juni. Apple iliipiku kampuni shindani za Silicon Valley kama vile Amazon na Microsoft na kuweza kufikia hadi thamani ya dola trilioni $1.

Tangu iPhone ilipowekwa sokoni kwa mara ya kwanza mwaka 2007, hisa za Apple zimekuwa zikipanda kwa 1,100% a na kuongezeka takriban mara tatu katika kipindi cha mwaka uliopita.Ongezeko hilo ni hata bora zaidi kwa kiwango cha 50,000% - tangu kampuni hiyo iliposajiliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1980.

Kiwango hicho kimepita ongezeko la 2,000% la kiwango cha S&P 500 katika kipindi sawia. Apple ilianzishwa na muasisi mwenza wa kituo cha kutengeneza magari Steve Jobs mnamo mwaka 1976 na mwanzo ilifahamika zaidi kama kutengeneza kpmyuta za kibinafsia aina ya Mac kabla ya soko lake la smartphone kufungua njia ya uchumi wa app.

Bwana Jobs, ambae alifariki dunia mwaka 2011 na kurithiwa na Mkurugenzi Mkuu Tim Cook, alisimamia maendeleo ya iPhone, ambayo ilibadili kabisa kipato cha Apple. Mnamo mwaka 2006 kampuni hiyo ilikuwa na mauzo ya chini ya $20bn na kutangaza faida ya takriban $2bn. Mwaka jana mauzo yake yalipanda hadi kufikia $229bn, na faida ya $48.4bn, na kuifanya kuwa kampuni yenye faida kubwa zaidi miongoni mwa makampuni ya Marekani.

PetroChina iliwahi kuwa na thamani ya trilioni $1.1 kwa kipindi kifupi baada ya kuendesha shughuli zake mjini Shanghai in 2007, licha ya kwamba nyingi kati ya hisa zake zilishikiliwa na serikali ya Uchina, kwa sasa inathamani ya takriban dola bilioni 220 ($220bn).

Licha ya kupata thamani ya trilioni $1 , wachanganuzi wa masuala ya kiuchumi bado hawaoni hisa za Apple kama ghali ikizingatiwa kwamba wanaendesha biashara ya takribani mara 15 ya faida iliyotarajiwa, ikilinganishwa na ile ya Amazon ambayo ni mara 82 na mara 25 ya Microsoft. Hali kadhalika kuongezeka kwa hisa za Apple katika miezi ya hivi karibuni ulikuwa ni uamuzi wa kampuni hiyo wa kutenga dola bilioni 100 ( $100bn) kununua hisa.

Uchambuzi uliofanywa na mwandishi wa masuala ya teknolojia nchini Marekani Dave Lee, Huenda yalikuwa malengo ya Steve Jobs kuifikisha Apple katika hatua hii, lakini ni thahiri kwamba ni uwezo wa kibiashara wa Tim Cook uliowawezesha kufika hapa walipo. Wakati masoko ya hisa ya makampuni mengine ya teknolojia yanahangaika, Apple iko mbele. Kupanda kwa hisa zake kumechochewa na mambo mawili muhimu. Inauza simu chache za iPhones, lakini kwa kutengenezasimu zenye gharama kubwa mwaka jana, imeweza kutengeneza pesa zaidi kwa simu.

Apple pia imebuni vyanzo vyake vya faida. Sasa inatengeneza karibu dola bilioni 10 ($10bn) kila miezi mitatu kutoka kwa huduma zake kama vile mauzo ya apps, hifadhi ya data pamoja na kupokea muziki kwa njia ya moja kwa moja.

Kampuni hiyo iliwaambia wawekezaji wiki hii kwamba inatarajia kumaliza kumaliza mwaka ikiwa imara zaidi ikisaidiwa , kwa hali ya kawaida na kutoa simu nyingine mpya ya iPhone.Masoko ya hisa yana ushindani mkubwa na tisho dogo lakini linakua kutoka kwa watengenezaji wa Kichina wa martphone yanaweza kuvuka viwango vya Apple katika miaka ijayo. Lakini hata kama utakuwa na maoni ya aina gani ya kampuni na bidhaa zake , vifaa vya Apple vimeibadilisha dunia- na leo imeweka historia ya kifedha pia.

Latest News

UFARANSA YATANGAZA KIFO CHA KIONGOZI WA AL-QAEDA.
06 Jun 2020 08:27 - Grace Melleor

Waziri wa Jeshi wa Ufaransa Florence Parly ametangaza kifo cha kiongozi wa al-Qaeda katika ukanda wa Maghreb (Aqmi) Abde [ ... ]

MZOZO WA SERIKALI YA LIBYA NA HAFTARI WAENDELEA KUSHIKA KASI.
06 Jun 2020 07:20 - Grace Melleor

Serikali ya Libya yadai kuuteka mji muhimu kutoka kwa hasimu wake Khalifa Haftar.

MPAKA WA HOLILI NA NAMANGA BADO KIZUNGUMKUTI.
05 Jun 2020 14:06 - Grace Melleor

Mipaka miwili ya Tanzania na Kenya eneo la Namanga na Holili imefungwa tena baada ya kuibuka hali ya sintofahamu kuhusu  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.