Star Tv

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema wanawake watamuweka madarakani rais mwanamke mwaka 2025.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo wakati akihutubia katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya demokrasia duniani jijini Dar es Salaam.

“Sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025, tukifanya vitu vyetu vizuri tukishikamana tukimweka rais wetu tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana, wameaanza kutuchokoza, kuandika kwenye vigazeti Samia hatasimama nani kawaambia?."-Amesema Rais Samia.

Rais Samia amesisitiza kuwa ikiwa fadhila za Mwenyezi Mungu zitakuja mikononi mwa mtu asiziache;

“Fadhila za Mungu zikija mikononi kwako usiziachie, hizi ni fadhila za Mungu ndugu zangu wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hizi, wanawake tumefanaya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hizi, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hizi leo Mungu ametupa baraka mikononi".

Aidha, Rais Samia amekabidhiwa tuzo tatu za heshima kutoka makundi mbalimbali ya wanawake nchini humo kwa kutambua mchango wake katika utetezi kwa wanawake kwenye maadhimisho haya ya siku ya Demokrasia Duniani.

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.