Star Tv

New Zealand imeripoti kile inachoamini kuwa kifo cha kwanza kinachohusisha chanjo ya corona aina ya Pfizer.

Bodi huru inayoangazia usalama wa chanjo nchini humo imesema kifo cha mwanamke huyo ''pengine'' ni kutokana na maumivu ya misuli ya moyo.

Pia imesema kulikuwa na changamoto nyingine ambazo kuna uwezekano zilisukuma athari za chanjo kutokea.

Waangalizi wa Ulaya wamesema kuwa ugonjwa huo ni ''nadra'' na kuwa faia ya chanjo ni kubwa zaidi kuliko athari maya za chanjo.

Hatahivyo, Bodi inayoshughulikia usalama wa chanjo ya Covid-19 imesema kuwa maumivu ya misuli ya moyo ''pengine yalitokana na chanjo".

"Hii ni kesi ya kwanza huko New Zealand ambapo kifo kimehusishwa na chanjo ya Pfizer COVID-19". Wakati Kituo cha Ufuatiliaji wa athari mbaya kimepokea ripoti nyingine za vifo kwa mtu aliyepewa chanjo ya hivi karibuni, lakini hakuna taarifa ya kifo inayohushwa na chanjo.

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.