Manchester City wanatarajiwa kutoa ofa mpya kwa mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, 29, na wanaamini kuwa Arsenal watamruhusu raia huyo wa Chile kuondoka mwezi huu.

Sanchez yuko tayari kurejesha kima cha pauni milioni 25 kuhakikisha kuwa amejiunga na Manchester City mwezi huu. (Sun)

Arsenal watamruhusu Sanchez kuondoka ikiwa watapokea hadi paui milioni 30 na wanataka shughuli hiyo kukamilika mapema ili kuwawezesha kumtafuta mchezaji ambaye atachukua mahala pake. (Mirror)

Taarifa zinasema kuwa Sanchez huenda akajiunga na Manchester City kwa muda wa wiki moja inayokuja. (Independent)

Arsenal wamemuorodhesha mshambuajia wa Monaco Thomas Lemar, 22, kuwa nambari moja katika kuchukua mahala pake Sanchez, baada ya kushindwa kumsaini mfaransa huyo msimu uliopita.Mirror

Valencia nao wako kwenye mazungumzo na Arsenal kuhusu Coquelin. (Cadena Ser - in Spanish)

Chelsea wamesitisha mikakati kwa kumwinda beki wa Juventus Mbrazil Alex Sandro, 26, kwa sababu klabu hiyo ya Italia inataka paunia milioni 60 kwa beki huyo. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 24, anasema yuko sawa katika klabu hiyo lakini ni lazima waanze kushinda vikombe kumwezesha kubaki. (Star)

Leicester wana nia ya kumuchia mshambuliaji Kelechi Iheanacho, 21, kuondoka mwezi huu licha ya kumsani mnigeria huyo tu hivi karibu kwa pauni milioni 25. (Sun)

West Ham wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa England na Newcastle Jonjo Shelvey, 25, kwa pauni milioni 12. (Express)

Juventus hawatamsaini kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 22, kwa sababu Paris St-Germain wanataka kutoa pauni milioni 150 kwa raia huyo wa Serbia ambaye pia amewavutia Manchester United. (Il BiancoNero - in Italian)

Newcastle watamruhusu mshambuliaji raia wa Serbia Aleksandar Mitrovic, 23, kuondoka Januari lakini wanataka kurejesha pauni milioni 18 walizotumia kumnunua miezi 18 iliyopita.

Kwa hisani ya BBC.

Latest News

RAW:Roman Reigns atetea mkanda wake wa munngano wa mabara
18 Jan 2018 10:19 - RobinLeah Madaha

Katika ulingo wa mieleka , mbabe wa mieleka Roman Reigns ametetea mkanda wake wa muungano wa mabara baada ya kuchapa wac [ ... ]

Masters 2018: Kryren Wilson ambwaga bingwa wa dunia mara mbili Barry Hawkins.
18 Jan 2018 10:12 - RobinLeah Madaha

Na katika mashindano ya mchezo wa Snuka ya Masters 2018 yanayoendelea katika Ukumbi wa Alexandra Palace huko mjini Londo [ ... ]

• FURSA YA KIUCHUMI: Uoteshaji miti wawanufaisha vijana wilayani Nzega
18 Jan 2018 10:02 - RobinLeah Madaha

Baadhi ya vijana wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora wameibua fursa ya kiuchumi ya uoteshaji miti kama njia ya kuwapatia ki [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.