Star Tv

Vijana wa kitanzania wanatakiwa kujenga utamaduni wa kupima mambo na kauli mbalimbali wanazoambiwa ili kujinusuru katika uvunjifu wa amani na kuliweka taifa katika hali ya Taharuki.

Akizungumza na vijana wa Zanzibar wakati akifungua kongamano la vijana kuhusiana na muungano na fursa za ajira kwa vijana wa Zanzibar waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais wa muungano Januari Makamba amewaeleza vijana hao kuwacha kufanya mambo kwa kukurupuka bali wawe makini na wapinga maendeleo ambao huja na vishawishi mbali mbali.

Anafafanua kuwa Muungano na mapinduzi ya Zanzibar ni urithi adhimu kwa mustakbali wa ustawi wa wananchi katika kukuza uchumi na kuimarisha maendeleo hivyo changamoto zinazojitokeza isiwe ndio chanzo cha kuukana muungano na mapinduzi bali watambue usatawi na fursa zinazopatikana ndio malengo ya ya Taifa la Tanzania.Pamoja na mambo mengine amelazimika kugusia mpango mkakati wa fursa za ajira kwa upande wa muungano ambapo amesema kuwa asilimia 21% hutolewa kwa upande wa Zanzibar Akizungumza wakati akitoa muhtasari wa fursa za ajira na malengo ya kongamano hilo Mkurugenzi Muungano Baraka B Baraka anasema kuwa vijana ni raslimali kubwa katika nchiyoyote endapo wakitumika ipasavyo.

Sekretarieti ya ajira serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inajaribu kutoa taaluma kwa vijana mbali mbali hasa kukabili mapungufu ya vijana katika kuomba ajira Mkuu wa kitengo cha mawasiliano sekretarieti ya ajira.

Baadhi ya vijana wakati wa kongamano hilo wanaona fursa za ajira za muungano kwao bado ni tatizo. Kongamano hilo lililowaashirikisha mabaraza ya vijana visiwani Zanzibar limefanyika wakati waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais Muungano na Mazingira Januari Makamba akiwa katika ziara yake visiwani Zanzibar.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.