Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala, amewasainisha Wakuu wa Wilaya wa Wilaya zote mkoani humo mikataba ya uwajibikaji katika Uhamasishaji wa Ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya pamoja na Uandikishaji wa Wananchi kwenye Bima ya Afya ya Jamii, CHF, ili kufanikisha Sera ya Serikali ya Afya ya Msingi.

Hata hivyo kwa Mkoa wa Mbeya kati ya vijiji 533, ni vijiji 233 tu ndivyo vyenye Zahanati sawa na asilimia 43.7 ya mahitaji halisi, wakati kati ya Kata 178 zilizopo mkoani hapa, ni kata 25 tu ndizo zenye vituo vya afya sawa na asilimia 14 ya mahitaji yaliyopo.

Mikataba hiyo imesainiwa na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za mkoani hapa ili iwe kigezo cha kuwabana katika utekelezaji wa lengo hilo la Serikali.

Kwa mujibu wa mikataba hiyo, Wakuu hao wa Wilaya wanatakiwa kuhakikisha ujenzi wa Zahanati na vituo hivyo vya Afya unakamika hadi ifikapo mwaka 202 Mkakati huo unaosimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya unakwenda sambamba na ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, CCM ya mwaka 2015 katika Kifungu cha 50(a), Kifungu kidogo cha kwanza cha ilani hiyo ambacho kimeaihidi ujenzi wa Zahanati katika kila kijiji na Ujenzi wa Kituo cha Afya katika kila kata endapo watanzania wangeipa ridhaa ya uongozi CCM ngazi ya Urais.

Picha na mtandao.

 

Latest News

MARUFUKU MICHANGO: Tabora wampongeza Rais Magufuli
19 Jan 2018 12:01 - RobinLeah Madaha

UMOJA wa Vijana wa CCM Mkoani Tabora,umempongeza Rais John Magufuli kwa hatua yake ya kupiga marufuku michango mbalimbal [ ... ]

Mtu afariki baada ya 'kuigonga' ndege Mwanza
19 Jan 2018 11:17 - RobinLeah Madaha

Mtu mmoja amefariki nchini Tanzania baada ya kuigonga ndege iliokuwa ikipaa katika uwanja wa ndege wa Mwanza. Akizungumz [ ... ]

Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 19.01.2018
19 Jan 2018 09:13 - RobinLeah Madaha

Mshambuliaji wa Stoke na Uingereza Peter Crouch, 36, analengwa kusajiliwa na Chelsea baada ya majeruhi kumnyima Andy Car [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.