Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni uliyowasilishwa na Waziri wa mambo ya nje wanchi hiyo mjumbe maalum Sam Kutesa ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda.

Akizungumza mara baada ya kuwasilisha ujumbe huo ikulu ya Dar es Salaam waziri huyo wa Uganda Sam Kutesa amesema Rais Museveni amemtumia Rais Magufuli na Watanzania wote salamu za heri ya mwaka mpya na pia wamezungumzia masuala yahusuyo uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda.

“Licha ya salamu za mwaka mpya lakini Tumezungumza namna nchi mbili hizo zitakavyokuza zaidi uhusiano katika maeneo mbalimbali, kama miradi ya maendeleo ya ushirikiano ukiwemo mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga hapa Tanzania”

Picha na mtandao.

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.