Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu miaka 30 jela watu watano akiwemo Mfanyabiashara Moriss Malianga maarufu kama ‘Rais wa Sinza’ baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unya’nganyi wa kutumia silaha.

Wengine waliohukumiwa ni pamoja na Flano Masulu (Singu), Jeremiah Mgori, Sandru Kamugisha na Sadick Bwanga. Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo amesema mahakama imeridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka ambao umethibitisha mashtaka dhidi yao.

Awali katika kesi hiyo namba 14 ya mwaka 2016, wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko aliomba wateja wake wapatiwe nafuu ya adhabu. Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa December 22, 2015 maeneo ya Mabibo Luhanga washtakiwa waliiba Dola za Marekani 8,600 ambayo ni sawa na Sh.Mil 18 kwa wakati huo.

Pia wanadaiwa waliiba tena Tsh milioni 2.5,  laptop moja na simu nne vyote vikiwa ni mali za Anderson Balongo na baada ya kuiba walimtishia kwa bastola Zeno Mriwa, Aneth Paulo, John Mkundi ili kujipatia mali hizo.

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.