Msako wa madawa ya kulelya kwa kutumia kikosi cha mbwa maalum wa Polisi wenye mafunzo ya kijeshi umeanza kuzaa matunda mkoani Singida, baada ya kufanikiwa kukamata viroba vya bangi iliyokuwa ikisafirishwa kwa basi kutoka Kahama-Shinyanga kwenda Jijini Dar-es-salaam.

Ilikuwa mapema asubuhi katika eneo la mzani barabara kuu ya Singida- Mwanza, wakati zoezi la ukaguzi wa magari mbalimbali lilipoanza ili kusaka madawa ya kulelya kwa kutumia kikosi cha mbwa wa Jeshi la Polisi wenye mafunzo maalum kwa ajili ya kufanya shughuli hiyo muhimu.

Hata hivyo baadaye jioni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Isaya Mbughi, akakutana na waandishi wa habari na kutoa taarifa za kufanikiwa kukamata viroba vya bangi kwenye basi la abiria.

Kaimu Kamanda Mbughi anasema ingawa mwenye bangi hiyo anadaiwa kupanda gari lingine, lakini polisi wanaendelea kuwashikilia mafundi wawili wa basi hilo ambao walikabidhiwa mzigo huo.

Wakati mwenye bangi bado anaendelea kutafutwa, mafundi wa basi waliokabidhiwa mzigo huo toka Kahama wanatarajiwa kupandishwa kizimbani wakati kwa ajili ya kujibu shitaka linalokabili.

Picha na mtandao.

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.