Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ameagiza kulipwa kwa madeni ya ndani yatakayokuwa yamehakikiwa kuanzia mwezi wa pili mwaka huu yakiwemo ya wazabuni mbalimbali waliotoa huduma katika taasisi za serikali,madai ya walimu pamoja na madai ya wakandarasi.

Rais Magufuli ametoa akizo hilo wakati akiagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Dkt Magufuli ameeleza kuwa serikali itatoa shilingi milioni 200 kwa ajaili ya kulipa madeni hayo na akasisitiza kwamba madeni yatakayolipwa ni ya ndani na ambayo yameahakikiwa na kutaka maandalizi ya kutoa fedha yaanze mara moja Kwa upande wake Gavana Mstaafu,Prof. Ndullu amesema miongozo muhimu ya serikali ya awamu ya tano imesaidia kuimarisha uchumi ikiwemo kudhibiti mfumuko wa bei ambao mwezi Novemba 2017 ulifikia asilimia 4.4 na kuongezeka kwa akiba ya fedha za kigeni kutoka Dola za Marekani Bilioni 1.8 hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 6 hivi sasa, hali ambayo imeimarisha uwezo wa Serikali kujiendesha na kugharamia miradi mikubwa ya maendeleo.

Naye Gavana Mteule Prof. Florens Luoga ameeleza kuwa taarifa zinazotolewa na benki kuu kuhusu ukuaji wa uchumi zinaandaliwa kitaalamu na kwa kushirikisha vyombo mbalimbali vikiwemo Benki ya Dunia,Shirika la Fedha la Kimataifa,IMF na ameonya dhidi ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakipotosha ukweli kuhusu takwimu za uchumi zinazotolewa na BOT.

Gavana mteule Pfofesa Luoga aliteuliwa kuwa gavana mpya mnamo Oktoba 23,2017,akiwa mjumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango,aina na thamani ya madini katika makinikia wakati wajumbe wa kamati hizo walipokuwa wakitunukiwa vyeti na Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

Picha na mtandao.

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.