Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa bado hawajakabidhiwa nyaraka walizoziomba kutoka kwa aliyekuwa Rais wa klabu ya Simba.

Evans Aveva anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha wa USD 300,000 ili wapate nyaraka za upelelezi.

Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa TAKUKURU, Leonard Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, pia upelelezi bado haujakamilika.

Pia Swai amedai kuwa bado hawajakabidhiwa nyaraka walizoziomba kutoka Ofisi ya Aveva ili wakamilishe upelelezi.

Hata hivyo, upande wa utetezi umeieleza mahakama kuwa wameipokea barua ya TAKUKURU kuhusu maombi hayo na wanayafanyia kazi.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi January 11,2018.

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.