Mwanamume mmoja amejipiga risasi na kujiua nje ya Ikulu ya Marekani ya White House mjini Washington, kikosi cha kumlinda rais kimesema Kikosi hicho kilisema kuwa mwanamume huyo alikaribia ua unaozunguka Ikulu katika barabara ya Pennsylvania kabla ya kuchomoa bunduki na kupiga risasi mara kadhaa.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa, kulingana na polisi. Rais Donald Trump hakuwa kwenye Ikulu. Yuko katika kasri lake la Mar-a-Lago huko Florida. Mwanamume huyo alikuwa kwenye watu wengi wakati alipiga risasi, kulingana na wale walioshuhudia. Video iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter ilionyesha watu wengi wakikimbia kutoka eneo hilo.

Kumekuwa na visa kadha vinavyohusu usalama katika Ikulu ya White House miaka ya hivi karibuni. Cha hivi karibuni tarehe 23 Februari, gari liliendeshwa kwenda kwa kizuizi cha Ikulu ambapo mwanamke wa miaka 35 alikamatwa.

Latest News

Trump akubali mualiko wa kukutana na Kim Jong Un
09 Mar 2018 12:20 - Mohamed Mnzava

Rais Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani  [ ... ]

Wanawake DRC wanapigania haki zao kumiliki ardhi
09 Mar 2018 12:15 - Mohamed Mnzava

Wanawake wanaoishi vijijini huko Jamhumuri ya Kidemokrasi ya Kongo, hawana haki ya urithi wa mali pamoja na ardhi iliyoa [ ... ]

Rais Kenyatta, Odinga wakutana, waapa kufanya kazi pamoja
09 Mar 2018 11:15 - Mohamed Mnzava

Kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya uliofanyika October 2017, na kuleta mkanganyiko mkubwa wa kisias [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.