Star Tv
Mwanamume aliyejibadilisha jinsia na kuwa mwanamke amefanikiwa kumyonyesha mtoto katika kisa cha kwanza cha iana yake kuwahi kushuhudiwa, watafiti wanasema. Mwanmke huyo mwenye umri wa miaka 30 alitaka kumnyonyesha mtoto baada ya mpenzi wake aliyejifungua kusema hataki kumnyonyesha mtoto huyo, hayoni kwa mujibu wa wa jarida la afya la watu waliojibadili jinsia. Alifanikiwa kunyonyesha baada ya kumeza dawa na kukamua maziwa, ripotihiyo inasema kutoka nchini Marekani. Mtaalamu wa Marekani anasema utafiti huo huenda ukachangia visa zaidi vya wanaume walijibadilisha jinsia kuwa wanawake kunyonyesha watoto. Mwanamke huyo aliyekuwa anapokea matibabu ya kubadili homoni zake mwilini kwa muda wa miaka 6, lakini hajafanyiwa upasuaji kubadili sehemu zake za siri, wakati alipowaomba madaktari wamsaidie atimize lengo lake la kumnyonyesha mtoto. Kabla ya mtoto huyo kuzaliwa, madakatari walimpadawa za miezi mitatu unusu kumsaidia kupata maziwa, kwa kawaida dawa hizo hupewa wanawake waliowaasili watoto au waliojipatia watoto kupitia wanawake wanobeba mimba kibiashara kuwaisaidia wasioweza kuzaa. Dawa hizo husisimua homoni mwilini kushinikiza kutoa maziwa na kuzuia homoni za kiume na pia alihitajika kukamua maziwa yake. Na mtokeo yake, yalimsababisha mwanamke huyo kuweza kupata maziwa kiasi. Watafiti wanasema mtoto huyo alikunywa maziwa hayo tuu kwa wiki zake sita za uhai, wakatiambapo ukuwaji wake, ulaji na uwendaji haja wake ulikuwa unaendelea kama kawaida. Baada ya hapa, mtoto alianza kupewa maziwa ya mkebe kwasababu maziwa yalianza kupungua. Mtoto huyo sasa ana miezi sita na anendelea kunyonya kama sehemu ya lishe yake, wahiriri wa utafiti huo wanasema.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.