Star Tv

Tetemeko la ukubwa wa 7.3 katika vipimo vya richa limekumba eneo la kaskazini mwa Iran na Iraq na kuua watu kadha.

Takriban watu 129 waliuawa katika mkoa ulio magharibi mwa Iran wa Kermanshah, kwa mujibu wa maafisa.

Tetemeko hilo lilizua hofu hadi kusababisha watu kukimbia kutoka manyumbani mwao kwenda barabarani.

Misikiti kwenye mji mkuu wa Iraq Baghdad, imekuwa ikifanya maombi kwa kutumia vipasa sauti.

Wengi wa waathiriwa walikuwa ni kwenye mji wa Sarpol-e Zahab, kilomita 15 kutoka mpakani.

Kulingana na kituo cha Marekani USGS tetekemo hilo lilitokea umbali wa kilomita 33.9 chini ya ardhi la lilisikika nchini Uturuki, Israel na Kuwait.Tetemeko hilo lilitokea kilimita 30 kusini magharibi mwa mji wa Halabja karibu na mpaka wa Iran.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.