Mshambuliaji wa Stoke na Uingereza Peter Crouch, 36, analengwa kusajiliwa na Chelsea baada ya majeruhi kumnyima Andy Carroll , 29, fursa ya kuhamia klabu hiyo.

(Telegraph) Chelsea inataka kumsajili mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko, 31, na beki wa Itali Emerson Palmieri, 23, kutoka Roma.

Wawili hao wanaweza kugharimu jumla ya £77m. (Daily Star) Chelsea itamtumia mshambuliaji wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 kumsajili Edin Dzeko. (Sky Italia) Kipa wa Manchester United David De Gea, 27, anasema kuwa katika klabu hiyo ni kitu maalum .

Raia huyo wa Uhispania alitaka kuzima uvumi ambao umekuwa ukisambaa kuhusu hatma yake katika uwanja wa Old Trafford.(ESPN) Manchester City wana hamu ya kiungo wa kati wa Liverpool na Ujerumani Emre Can, 24, lakini hatma yake huenda ikategemea hatua ya Liverpool ya kutaka kumsajili kiungo wa Schalke, 22 Leon Goretzka.

(Mirror) Tottenham inashindana na Manchester United katika mpango wa kutaka kupata saini ya mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazilian Lucas Moura, 25. (L'Equipe - in French) Alexis Sanchez amelazimika kufanya mazeozi na timu ya vijana huku mpango wa mchezaji huyo kuelekea Old Trafford ukiendelea kuchelewa.

(Times) United wanaiongoza Liverpool na Chelsea katika harakati za kumnunua kiungo wa kati wa Nice Jean-Michael Seri, 26, huku Manchester City pia ikimtaka mchezaji huyo wa Ivory Coast. (Mirror) Chelsea huenda ikakabiliwa na marufuku ya uhamisho kwa kukiuka sheria kuhusu usajili wa wachezaji wa kigeni walio na chini ya umri wa miaka 18.

(Guardian) Brighton inamtaka mshambuliaji wa Uholanzi na PSV Jurgen Locadia, 24. (De Telegraaf - in Dutch) Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 24, atalazimilka kuwasilisha ombi la uhamisho ili kupata fursa ya kujiunga na Manchester United, kulingana na afisa mkuu wa Juventus Beppe Marotta.

(La Gazetta Dello Sport - in Italian) Arsenal imepiga hatua kubwa katika kumsajili mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang baada ya mchezaji huyo ,28, kutohusishwa katika kikosi cha timu hiyo dhidi ya Hertha Berlin. (Bild - in German)

Kwa hisani ya BBC.

Latest News

Amtumia ndugu yake kutoroka jela
14 Feb 2018 14:15 - Mohamed Mnzava

Mamlaka nchini Peru zimemkamata mfungwa zaidi ya mwaka mmoja tangu atoroke jela kwa kumuacha ndugu yake pacha katika naf [ ... ]

Ukame Cape Town umekuwa 'Janga la kitaifa'
14 Feb 2018 14:05 - Mohamed Mnzava

Afrika kusini imetangaza ukame unaoshuhudiwa Cape Town - mji unao elekea kuishia bila ya hata tone la maji - kuwa janga  [ ... ]

Waziri Mwigulu azungumzia kampeni kuhusishwa na tukio la Mbunge Lissu
14 Feb 2018 13:51 - Mohamed Mnzava

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kesi ya kuumwa kwa Mbunge wa Singida [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.