Mkufunzi wa Everton Sam Allardyce anasema kuwa klabu hiyo imeanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott kwa mkataba wa kudumu.

Allardyce anataka kuimarisha safu yake ya mashambulizi na akasema kuwa Walcott mwenye umri wa miaka 28 atakuwa kiungo muhimu.

''Hatujakubaliana lakini mazungumzo yanaendelea na tuna matumaini ya kumuajiri kwa mkataba wa kudumu'', alisema Allardyce, 63. "Sijipatii matumaini nisije nikashangazwa.

Nitafurahi sana iwapo mtu yeyeote hata iwapo sio Walcott atatia saini kanadarasi.

Allardyce, ambaye tayari amemsajili mshambuliaji Cenk Tosun kutoka Besitkas kwa kitita cha £27m mwezi Januari, amesifu kasi ya Walcott, uzoefu na uwezo wake wa kupiga krosi nzuri kuwa mchango atakaoleta katika klabu yake.

Kwa hisani ya BBC.

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.