Wanaume watatu nchini Zambia wamelazwa kwa makosa katika wadi ya wagonjwa wa kipindupindu baada ya kunywa dawa za asili zinazodaiwa kuongeza nguvu za kiume. Kiongozi wa mkoa, Chanda Kasolo, amesema kuwa mara baada ya kunywa dawa hizo, walianza kutapika kitu ambacho kilisababishwa na mchanganyiko wa chakula, pombe na dawa hizo za asili. ''Baada ya majibu ya vipimo kupatikana , inaonekana kuwa mchanganyiko wa pombe, vyakula na dawa hiyo, ulisababisha mchafuko wa mfumo wa chakula na hivyo ikahusishwa na kipindupindu lakini baada ya kuwauliza maswali, baadaye walikiri kuwa walikunywa dawa ya kuongeza nguvu katika tendo la ndoa'' Wagonjwa hao bado wapo katika kituo hiko cha kipindupindu na wanaendelea vizuri na matibabu, aliongeza bwana Kasolo.Wanaume hao watatu wanatoka katika mji mdogo wa katete, na si wagonjwa wa kipindupindu bali walikunywa dawa ya kuongeza nguvu ya kufanya tendo la ndoa inayojulikana kama Mvubwe. Ugonjwa wa kipindupindu uliolipuka mwaka jana ulisababisha vifo vya watu takribani 70, kusini mwa Afrika. Rais Edgar Lungu mwezi uliopita, alitoa agizo kwa jeshi la Zambia kusafisha maeneo ya masoko na kuondoa uchafu ambao ndio saabu ya kipindupindu.

Latest News

Amtumia ndugu yake kutoroka jela
14 Feb 2018 14:15 - Mohamed Mnzava

Mamlaka nchini Peru zimemkamata mfungwa zaidi ya mwaka mmoja tangu atoroke jela kwa kumuacha ndugu yake pacha katika naf [ ... ]

Ukame Cape Town umekuwa 'Janga la kitaifa'
14 Feb 2018 14:05 - Mohamed Mnzava

Afrika kusini imetangaza ukame unaoshuhudiwa Cape Town - mji unao elekea kuishia bila ya hata tone la maji - kuwa janga  [ ... ]

Waziri Mwigulu azungumzia kampeni kuhusishwa na tukio la Mbunge Lissu
14 Feb 2018 13:51 - Mohamed Mnzava

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kesi ya kuumwa kwa Mbunge wa Singida [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.