Mwanasoka Didier Drogba, mwenye asilia ya Ivory Coast, amefungua shule ya kwanza ya msingi. Shule hiyo inatarajiwa kuwasaidia maelfu ya watoto walioko vijijini kwenye mashamba ya kakao ya jamii ya Pokou-Kouamekro kupata elimu bora imearifiwa.

Katika sherehe za ufunguzi wa shule hiyo, Drogba alisema, tumeshughulika na mradi huu kwa miaka miwili na ninayo fahari kuona umekamilika.

Imani ya shirika langu daima imekuwa mara zote watoto wakipata fursa ya kupata elimu bora na huduma za afya zilizo bora, tutajenga kizazi chenye madaktari, wanasayansi, wafanya biashara wa kiume na wa kike na ndivyo tutakavyo ijenga Afrika iliyo bora zaidi.

Shule hiyo imejengwa chini ya ufadhili wa shirika la Didier Drogba, kwa ushirikiano mkubwa na kampuni ya Nestlé na mpango wa kimataifa wa uimarishaji zao la kakao .

Shule hiyo ina idadi ya vyumba vya madarasa sita, darasa la awali, kantini , maliwato, uwanja wa soka na nyumba za waalimu watatu.

Kwa hisani ya BBC.

Latest News

Amtumia ndugu yake kutoroka jela
14 Feb 2018 14:15 - Mohamed Mnzava

Mamlaka nchini Peru zimemkamata mfungwa zaidi ya mwaka mmoja tangu atoroke jela kwa kumuacha ndugu yake pacha katika naf [ ... ]

Ukame Cape Town umekuwa 'Janga la kitaifa'
14 Feb 2018 14:05 - Mohamed Mnzava

Afrika kusini imetangaza ukame unaoshuhudiwa Cape Town - mji unao elekea kuishia bila ya hata tone la maji - kuwa janga  [ ... ]

Waziri Mwigulu azungumzia kampeni kuhusishwa na tukio la Mbunge Lissu
14 Feb 2018 13:51 - Mohamed Mnzava

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kesi ya kuumwa kwa Mbunge wa Singida [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.