Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku anazungumza na mawakili wake kuhusu madai yaliotolewa na mmiliki wa Everton Farhad Moshiri kwamba aliamua kuondoka katika klabu hiyo baada ya kupata ''ujumbe wa uchawi''.

Moshiri aliuambia mkutano wa wamiliki wa hisa katika klabu hiyo kwamba Lukaku mwenye umri wa miaka 24 alipokea ujumbe huo baada ya kuzuru Afrika.

Lukaku alijiunga na United kwa pauni milioni 75 mwezi Julai baada ya kukataa kandarasi mpya Everton.

Mwakilishi wa mchezaji huyo aiambia BBC michezo kwamba uamuzi wa Lukaku haukushinikizwa na uchawi.

Msemaji huyo aliongezea: Hapendi kufuata imani kama hizo na sasa anatathmini hatua za kisheria anazoweza kuchukua.

BBC michezo inaelewa kwamba raia huyo wa Ubelgiji amekasirishwa na madai hayo.

Wawakilishi wake wanasema kuwa Lukaku alikataa kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi katika historia ya klabu ya Everton ili kuweza kucheza katika klabu kubwa duniani.

Wawakilishi wake waliongezea: Romelu ni mfuasi wa kanisa katoliki na kwamba haamini uchawi. Hakuwa na imani na Everton mbali na mradi wa bwana Moshiri.

Hiyo ndio sababu hakutaka kutia kandarasi nyengine.

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.