Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amemfuta kazi Inspekta mkuu wa polisi, Kale Kayihura na waziri wa Ulinzi, Henry Tumukunde. Generali Kayihura, ambaye ni mkereketwa wa vita vilivyomsaidia rais Museveni kuingia madarakani mwaka 1986, kwa wakati mmoja alikisiwa kuwa afisa mwenye mamlaka makubwa zaidi katika jeshi la Uganda.

Lakini amekabiliwa na shinikizo kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu wa usalama. Zaidi ya wanawake 20 wameuawa katika visa vya mauaji ambavyo havijatatuliwa katika maenoe yanayouzunguka mji mkuu wa Kampala, na katika miezi mitatu iliyopita raia watatu wa kigeni pia wameuawa. Naibu wake Okoth Ochola anashikilia wadhifa huo.

Kwa mujibu wa ujumbe alioandika rais Museveni katika mtandao wa Twitter, amesema: " Kwa uwezo wa mamlaka niliyopewa kikatiba, nimemteua Jenerali Elly Tumwiine kama waziri wa usalama. Nimemteua pia bwana Okoth Ochola kama afisa mkuu wa polisi. Niabu wake atakuwa ni Brigedia Sabiiti Muzeei.

Mnamo Mei mwaka 2017 Rais Museveni alimteua upya Kayihura kama mkuu wa polisi kwa muhula mwingine wa miaka mitatu,hadi mwaka 2020. Uteuzi huo ulikumbwa na mzozo na haukudumu.

Latest News

Trump akubali mualiko wa kukutana na Kim Jong Un
09 Mar 2018 12:20 - Mohamed Mnzava

Rais Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani  [ ... ]

Wanawake DRC wanapigania haki zao kumiliki ardhi
09 Mar 2018 12:15 - Mohamed Mnzava

Wanawake wanaoishi vijijini huko Jamhumuri ya Kidemokrasi ya Kongo, hawana haki ya urithi wa mali pamoja na ardhi iliyoa [ ... ]

Rais Kenyatta, Odinga wakutana, waapa kufanya kazi pamoja
09 Mar 2018 11:15 - Mohamed Mnzava

Kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya uliofanyika October 2017, na kuleta mkanganyiko mkubwa wa kisias [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.