Kiongozi wa Chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa chama kitafanya uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya Rais Jacob Zuma. Akizungumza kaika mkutano wa hadhara mjini Cape Town, Ramaphosa amedokeza kuwa Rais Zuma atatakiwa kujiuzulu. Amesisitiza kuwa wala rushwa wote wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria, kitu ambacho anasema Nelson Mandela, baba wa taifa hilo angekitaka. Bwana Ramaphosa alikuwa akizungumza katika kumbukumbu ya miaka 28 toka Rais wa kwanza mzalendo nnchini humo Nelson Mandela alipolihutubia taifa, mara tu baada ya kuachiwa gerezani. Kwa hisani ya BBC.

Latest News

Amtumia ndugu yake kutoroka jela
14 Feb 2018 14:15 - Mohamed Mnzava

Mamlaka nchini Peru zimemkamata mfungwa zaidi ya mwaka mmoja tangu atoroke jela kwa kumuacha ndugu yake pacha katika naf [ ... ]

Ukame Cape Town umekuwa 'Janga la kitaifa'
14 Feb 2018 14:05 - Mohamed Mnzava

Afrika kusini imetangaza ukame unaoshuhudiwa Cape Town - mji unao elekea kuishia bila ya hata tone la maji - kuwa janga  [ ... ]

Waziri Mwigulu azungumzia kampeni kuhusishwa na tukio la Mbunge Lissu
14 Feb 2018 13:51 - Mohamed Mnzava

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kesi ya kuumwa kwa Mbunge wa Singida [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.