Shirikisho la soka Tanzania TFF limemfungia kwa muda wa mwaka mmoja na faini ya shilingi milioni tatu mwenyekiti wa timu ya Abajaro Edger Chibula, baada ya kukutwa na kosa la utovu wa nidhamu. Chibula amekutwa na hatia baada ya kuzungumza maneno yasiyo sahihi kwa Tff alipofanya mahojiano na kituo kimoja cha redio hapa nchini. Kwa upande mwingine shirikisho hilo limesikitishwa na kitendo cha golikipa wa timu ya shupavu Fc ya morogoro khalifa Mgwila ambae alisema kushindwa kwenye mchezo dhidi ya Azam kumetokana na kutopewa fedha zao za maandalizi ya mchezo huo wa kombe la FA, katika mchezo huo Shupavu ilifungwa mabao 5 –0 Nayo bodi ya ligi kupitia kwa mtendaji wake mkuu Boniface Wambura imeweka usawa wa utumiaji wa uwanja wa Uhuru na Taifa kwa michezo ya Simba na Yanga .

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.