Manchester City wanatarajiwa kutoa ofa mpya kwa mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, 29, na wanaamini kuwa Arsenal watamruhusu raia huyo wa Chile kuondoka mwezi huu.

Sanchez yuko tayari kurejesha kima cha pauni milioni 25 kuhakikisha kuwa amejiunga na Manchester City mwezi huu. (Sun)

Arsenal watamruhusu Sanchez kuondoka ikiwa watapokea hadi paui milioni 30 na wanataka shughuli hiyo kukamilika mapema ili kuwawezesha kumtafuta mchezaji ambaye atachukua mahala pake. (Mirror)

Taarifa zinasema kuwa Sanchez huenda akajiunga na Manchester City kwa muda wa wiki moja inayokuja. (Independent)

Arsenal wamemuorodhesha mshambuajia wa Monaco Thomas Lemar, 22, kuwa nambari moja katika kuchukua mahala pake Sanchez, baada ya kushindwa kumsaini mfaransa huyo msimu uliopita.Mirror

Valencia nao wako kwenye mazungumzo na Arsenal kuhusu Coquelin. (Cadena Ser - in Spanish)

Chelsea wamesitisha mikakati kwa kumwinda beki wa Juventus Mbrazil Alex Sandro, 26, kwa sababu klabu hiyo ya Italia inataka paunia milioni 60 kwa beki huyo. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 24, anasema yuko sawa katika klabu hiyo lakini ni lazima waanze kushinda vikombe kumwezesha kubaki. (Star)

Leicester wana nia ya kumuchia mshambuliaji Kelechi Iheanacho, 21, kuondoka mwezi huu licha ya kumsani mnigeria huyo tu hivi karibu kwa pauni milioni 25. (Sun)

West Ham wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa England na Newcastle Jonjo Shelvey, 25, kwa pauni milioni 12. (Express)

Juventus hawatamsaini kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 22, kwa sababu Paris St-Germain wanataka kutoa pauni milioni 150 kwa raia huyo wa Serbia ambaye pia amewavutia Manchester United. (Il BiancoNero - in Italian)

Newcastle watamruhusu mshambuliaji raia wa Serbia Aleksandar Mitrovic, 23, kuondoka Januari lakini wanataka kurejesha pauni milioni 18 walizotumia kumnunua miezi 18 iliyopita.

Kwa hisani ya BBC.

Latest News

Trump akubali mualiko wa kukutana na Kim Jong Un
09 Mar 2018 12:20 - Mohamed Mnzava

Rais Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani  [ ... ]

Wanawake DRC wanapigania haki zao kumiliki ardhi
09 Mar 2018 12:15 - Mohamed Mnzava

Wanawake wanaoishi vijijini huko Jamhumuri ya Kidemokrasi ya Kongo, hawana haki ya urithi wa mali pamoja na ardhi iliyoa [ ... ]

Rais Kenyatta, Odinga wakutana, waapa kufanya kazi pamoja
09 Mar 2018 11:15 - Mohamed Mnzava

Kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya uliofanyika October 2017, na kuleta mkanganyiko mkubwa wa kisias [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.