Mnadhimu mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema Bw Tundu Lissu amesema dalili zinaonesha watu waliomshambulia kwa risasi mjini Dodoma mwaka jana walikuwa na uhusiano na serikali. Bw Lissu, akihutubia wanahabari kwa mara ya kwanza tangu kulazwa hospitalini, ameonekana kuilaumu serikali ya Rais John Magufuli kwa kuwakandamiza wapinzani.

Amesema anaamini shambulio dhidi yake lililenga kumnyamazisha kutokana na uokosoaji wake wa mara kwa mara wa serikali. Bw Lissu alikuwa akihutubu kutoka hospitali ya Nairobi jijini Nairobi ambapo amekuwa akipokea matibabu kwa miezi minne sasa.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati akisema hali nchini Tanzania imebadilika sana.Bw Lissu amesema kufikia sasa anaamini hakuna uchunguzi wa maana kuhusu kushambuliwa kwake mnamo 7 Septemba unaendelea.

Aidha, amesema Rais John Magufuli, ingawa aliandika ujumbe kwenye Twitter na pia kumtuma makamu wake Samia Suluhu Hassan, hajawahi kuzungumzia hadharani kisa cha kushambuliwa kwake.

"Tanzania imebadilika na kuwa taifa ambalo hakuna aliye salama. Mawakili wanaweza kurushiwa mabomu kwa kuwawawkilisha wateja wao. Nchi ambayo afisi za mawakili zinaweza kuvamiwa, na mawakili kufungwa jela," amesema Lissu.

Bw Lissu amesema amepona na kwamba anashukuru Mungu na wote waliomtakia uponaji wa haraka.

Kwa hisani ya BBC.

Latest News

MARUFUKU MICHANGO: Tabora wampongeza Rais Magufuli
19 Jan 2018 12:01 - RobinLeah Madaha

UMOJA wa Vijana wa CCM Mkoani Tabora,umempongeza Rais John Magufuli kwa hatua yake ya kupiga marufuku michango mbalimbal [ ... ]

Mtu afariki baada ya 'kuigonga' ndege Mwanza
19 Jan 2018 11:17 - RobinLeah Madaha

Mtu mmoja amefariki nchini Tanzania baada ya kuigonga ndege iliokuwa ikipaa katika uwanja wa ndege wa Mwanza. Akizungumz [ ... ]

Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 19.01.2018
19 Jan 2018 09:13 - RobinLeah Madaha

Mshambuliaji wa Stoke na Uingereza Peter Crouch, 36, analengwa kusajiliwa na Chelsea baada ya majeruhi kumnyima Andy Car [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.