Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa klabu yake haingefunga bao hata kama ingecheza kwa saa kumi baada ya upande wake kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Newcastle. Bao la dakika ya 65 la Matt Ritchie lilisababisha The Red Devils kushindwa kwa mara ya tano msimu huu. Sasa Manchestrer United wako nyuma ya viongozi Manchester City kwa pointi 16. "Miungu yao ya kanndanda ilikuwa wazi nao," aliseam Mourinho. "Haingewezekana leo." Meneja huyo wa zamani wa Chelsea alisema kuwa Newcastle walicheza kama wanyama kushinda nyumbani kwa mara ya kwanza tangu Oktoba. "Hisia zangu ni kuwa tungecheza kwa saa 10 na hatungefuga bao," alisema. "Tulikuwa na fursa wakati tulikuwa 0-0, alisema Mourinho, Alexis Sanchez alikuwa na fursa ya kufunga na kisha fursa zingine dakika za 20 na 25 za mwisho Free-kick ambayo ilichangia bao lake Ritchie, iliptikana wakati beki wa Manchester United Chris Smalling alilaumiwa kwa kuruka. Kwa hisani ya BBC.

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.