Star Tv

Everton imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot katika mkataba ulio na thamani ya £20m katika kandarasi ya miaka mitatu na nusu. Walcott, 28, ni mchezaji wa pili kusajiliwa na mkufunzi wa Everton Sam Allardyce katika dirisha la uhamisho la Januari baada ya mshambuliaji Cenk Tosun aliyesajiliwa kwa dau la £27m kutoka Besiktas.

Hatua hiyo inakamilisha huduma za Walcot za miaka 12 katika klabu hiyo ambapo alifunga magoli 108 katika mechi 397 "Kuna kitu muhimu kuhusu uhamisho huu najihisi vyema sana'', alisema Klabu ya zamani ya Walcott Southampton pia walikuwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo.

Lakini Walcott, ambaye hajaanza mechi yoyote ya ligi ya Arsenal msimu huu anaamini kwamba Allardyce anaweza kuimarisha mchezo wake. ''Nilihisi kwamba ni wakati nilifaa kuondoka'', alisema. Ni uchungu lakini ni vyema na nataka kuimarisha mchezo wangu na kuisaidia Everton kushinda mataji kama ilivyokuwa awali.

Aliongezea: Mkufunzi amekasirika lakini hiki ndicho nilichotaka. ''Nilizungumza naye na nilihisi hasira aliyokuwa nayo na kile alichotaka kutoka kwangu''. Katika taarifa yake , Arsenal ilisema: Sote tunamshukuru Walcott kwa mchango wake kwa Arsenal na tunamtakia kila la kheri.

Kwa hisni ya BBC

Latest News

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Urusi Kuchagiza Maendeleo Afrika kupitia Nishati ya Nuklia na Madini ya Urani
12 Aug 2023 10:07 - Kisali Shombe

ROSATOM, taasisi ya nishati ya nyuklia ya serikali ya Urusi ambayo iliwaalika zaidi ya waandishi wa habari 15 kutoka nch [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.