Home Blog

Majaliwa: Viwanda havitasimama kwasababu ya migogoro

SERIKALI imesema kuwa haita kubali kuendelea kusimamisha viwanda kwa sababu wa migogoro baina ya viwanda hivyo na vyama vya ushirika kwa maslahi ya watu wachache na kuwa viwanda vitaendelea kufanyakazi wakati matatizo yakishighulikiwa na serikali.

Kauli hiyo inatolewa na waziri Mkuu wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa ambayo ameitoa alipo tembelea kwenye kiwanda cha Chai cha Lupembe mkoani Njombe ambacho kilisimama kwa muda na kusababisha miundombinu yake na mali zake kudaiwa kuhujumiwa.

Waziri mkuu baada ya kutembela kiwanda hichi anakutananna wananchi wa kijiji cha Igombola  ambapo anasema kuwa wanakulima waendelee kulima chai na kupeleka kiwandani hapo kwa kuwa hakitasimama.

Imeandikwa na Furaha Eliabu.

Bei ya nafaka yapanda Mbeya.

BEI ya mazao aina ya nafaka katika baadhi ya masoko jijini Mbeya imepanda ikilinganishwa na bei za mazao hayo katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.

Wananchi waandamana kukosa maji baada ya mhudumu wa maji kukamatwa na DC

 

Na, Ahmed Makongo, Bunda;

WANANCHI wa kitongoji cha Mashine ya Maji katika kata ya Bunda stoo, mjini Bunda mkoani Mara, jana wamepiga yowe na kuanadamana kwa kukusanyika pamoja katika kituo cha Mashine ya kusukuma maji, iliyoko katika eneo la Migungani, mjini humo, kutokana na kituo hicho kufungwa na kusababisha kukosa huduma ya maji, kwa siku nzima ya jana.

Wananchi hao walifikia hatua hiyo baada ya kufika asubuhi katika eneo hilo, kwaajili ya kupata huduma hiyo ya maji na ndipo, wakakuta kituo hicho kimefungwa kwa kile kinachodaiwa kuwa mhudumu wa kituo hicho, ambaye ni mtumishi wa Idara ya maji, amekamatwa na polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili.

Ni kufuatia wananchi hao kufurika katika eneo hilo na kupaza sauti zao wakilalamikia kitendo hicho cha kukosa huduma hiyo ya maji mwenyekiti wa kitongoji cha Mashine ya Maji, Bw. Daud Kusekwa, amefika katika eneo la tukio kwa ajili ya kuwatuliza wananchi hao, ambao walikuwa na jazba, wakidai kuwa mhudumu wa kituo hicho amekamatwa bila kuwa na kosa lolote hivyo ni vyema akaachiwa uru.

Hali hiyo ya malalamiko ya wananchi hao ndiyo inayomfanya mwenyekiti huyo wa kitongoji kuamua kumuita afisa mtendaji wa kata ya Bunda Stoo, Bw. Raymond Bukombe na meneja wa mamlaka ya maji katika halmashauri ya mji wa Bunda, Injinia Mandemla Mansour, ambao wamefika katika eneo la tukio na kushuhudia umati mkubwa wa wananchi wengi wao wakiwa ni wanawake, waliokuwa tayari na vifaa vya kuchotea maji, lakini wakakosa huduma hiyo kutokana na kituo hicho kufungwa.

Hata hivyo, wananchi wa eneo hilo wakiongozwa na mwenyekiti wa kitongoji hicho, Bw. Daud Kusekwa, wamemuomba mkuu wa wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili, kuruhusu polisi wamuachie huru mtumishi wa idara ya maji.

Sikonge waaswa kutodharau zao za muhogo.

Wakazi Wilayani Sikonge, wameaswa kuondokana na dhana kuwa mazao ya muhogo na mtama ni kwa ajili ya watu maskini au wenye njaa.

Wameelezwa kuwa mazao hayo ni mazao mazuri kama mengine lakini yakiwa na faida ya kuhimili ukame na ndio maana yanahimizwa kulimwa.

Zao la muhogo ndio zao linaloweza kuliwa katika hali tofauti ikiwemo baada ya kuchomwa, kukaangwa na kupikwa huku likihitaji mvua kidogo.

Pamoja na kuhimizwa kulima zao hilo mazao mengine yanalimwa na hali sio mbaya.

Mkuu huyo wa wilaya pia alitembelea soko la Sikonge kujionea mazao yaliyopo na kuridhika kuwa hali ni nzuri ambapo wafanyabiashara walikuwa wakifanya biashara zao kama kawaida.

Imeandikwa na Robert Kakwesi

Picha: Mtandao

Waziri Mkuu Majaliwa atua Iringa tayari kwenda Njombe.

​Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ametua leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa Nduli mkoani Iringa tayari kuelekea mkoani Njombe kuendelea na ziara ya kikazi katika mkoa huo.

Mhe. Majaliwa alilazimika kukatiza ziara yake mkoani njombe na kwenda Dar Es Salaam kwa shughuli ya kikazi.

Mkoani Iringa Waziri Mkuu amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza.

YURO MILIONI 3 zatengwa kwaajili ya mradi wa nishati mbadala Zanzibar

Kiasi cha yuro milioni tatu zinategemewa kutumika katika kufanikisha  upembuzi yakinifu wa mradi wa kutafuta umeme mbadala kwa zanzibar wa upepo na nishati ya jua ili kukabiliana na changamoto ya kutegemea umeme wa mfumo mmoja tu wa kutumia cable kutoka Tanzania Bara.

Fedha hizo kutoka Jumuiya ya Ulaya zinategemewa kuiwezesha Zanzibar kuwa na njia nyengine ya kupata nishati hiyo ambapo inakisiwa inaweza kupunguza gharama katika matumizi yake kwa wananchi.

Akizungumza mara baada ya warsha kwa wadau mbali mbali kuhusina na kujenga uwelewa namna ya uendeshaji na ufuatiliaji wa mradi huo visiwani zanzibar Naibu Katibu Mkuu wizara ya Ardhi Maji, Nishati na Mazingira, Tahir Mohammed anasema kuwa hiyo ni fursa adhimu kwa zanzibar ambapo kwa kipindi kirefu Zanzibar haina uhakika wa upaikanaji wa nishati ya umeme kwa vile inatumia njia moja pekee  kutoka Tanzania Bara,

Meneja mradi huo kutoka shirika la umeme  Maulid Shirazi anasema kuwa watafanya utafuti wa kutosha na upembuzi yakinifu ili kuhakikisha kuwa inapatikana njia sahihi ya kupata umeme mbadala itakayoiwezesha Zanzibar kupata umeme wa uhakika sambamba na kutawanya elimu kwa jamii ili nao watambuwe mradi huo ambao tayari wameshaainisha maeneo ya kufunga minara.

Mada mbali mbali zimewasilishwa wakati wa warsha hiyo ambapo pia wadau walipata nafasi ya kuuliza na na kutoa michango ambayo kwa namna moja ama nyengine itafanikisha mradi hiyo.

Imeandikwa na Abdalla Pandu, Star TV – Zanzibar

Mtibwa Sugar yaiondosha Polisi Moro kombe la FA

Timu ya maafande wa Polisi Morogoro inayoshiriki ligi Daraja la Kwanza ngazi ya Taifa, imetupwa nje ya michuano ya kombe la Shirikisho, baada ya kushindwa kutamba mbele ya mahasimu wao, wakata miwa Turiani timu ya Mtibwa Sugar, kupitia mikwaju ya Penati.

Mchezo huo ulimalizika kwa timu zote mbili kutoka sare ya goli mbili kwa mbili na kuingia kwenye mikwaju penati, ambapo timu zote ziliweza kupiga penati saba huku polisi Moro wakikosa penati 3 na Mtibwa Sugar wakikosa penati mbili, hivyo kufanikiwa kuendelea raundi inayofuata ya michuano hiyo.

Mtangane huo uliowakutanisha mahasimu hao, umepigwa katika dimba la uwanja wa Jamhuri Morogoro,ambapo mpaka dakika tisini za Mwamuzi zinamalizika, Timu zote mbili ziliweza kutoka sare ya goli mbili kwa mbili na kufanikiwa kuingia kwenye mikwaji ya penati.

Bahati iliweza kuwaangukia wakata miwa wa Turiani, Mtibwa Sugar, mara baada ya kufanikiwa kushinda mtanange huo kwa kushinda penati tano dhidi ya nne za Polisi Morogoro.

Kufuatia ushindi wa Leo timu ya mtibwa  imefanikiwa kuendelea katika raundi inayofuata ya Michuano ya Shirikisho, huku ikijiandaa na mchezo wa ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya ndugu zao Kagera Sugar, na Polisi Moro wao wakijiandaa kuvaana na Kurungezi, mchezo utakaopigwa Januari 28 huko Mafinga.

Imeandikwa na Jackson Monela.

Bodaboda watakiwa kuwafichua wahalifu.

JESHI la polisi mkoa wa kipolisi wa Tarime na Rorya limeutaka umoja wa wafanyabiashara ya kusafirisha abiria kwa kutumia pikipiki maarufu kwa jina bodaboda wilayani Tarime mkoani mara kuwafichua waendesha pikipiki wanao fanya vitendo vya uharifu nyakati za usiku ukiwemo ubakaji wa wanawake na kukimbia na pesa za chenchi za wateja.

kauli hiyo imetolewa na mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Tarime, Anthon Kahema wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya waendesha pikipiki wilayani humo.

Imeandikwa na Jumanne Ntono

Watuhumiwa TASAF wakamatwa.

Takribani kaya 50 za wilayani Kalambo mkoani Rukwa zimeamriwa kukamatwa mara moja zikituhumiwa  kunufaika na fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kinyume na malengo ya mradi wa kusaidia kaya masikini.

SERIKALI: Tunatambua mchango wa sekta binafsi.

  1. SERIKALI imesema kuwa inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa nchi na kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano na sekta hiyo ili kuharakisha maendeleo ya wananchi kupitia sekta ya viwanda na biashara.